Ni wajibu kwa mwanamke kuvaa vifuniko vya mikoni (Gloves)


Swali: Ipi hukumu ya vifuniko vya mikono (gloves) pindi mwanamke anapotoka nyumbani?

Jibu: Ndio, tumeshatangulia kusema ya kuwa ni wajibu kwake kuufunika mwili wake wote. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayh wa sallam) anasema:

“Mwanamke ni ´Awrah (uchi), Pindi anapotoka nje, matumaini ya Shaytwaan huongezeka.”

Huenda mwanaume akafitinishwa na mwanamke vile vile akafitinishwa, kama livyosema mshairi ya kwamba chanzo cha yote ni mtazamo… Wajibu kwa mwanamke ni yeye awe amejisitiri, na akiweza kubaki nyumbani ni bora kwake. Uislamu umekuja kumhifadhia heshima yake, damu yake na mali yake. Lakini Waislamu wengi leo, wao ndio ambao wamepuuza mafunzo haya yenye baraka.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.net/default_ar.aspx?id=2972
  • Imechapishwa: 24/02/2018