Ni wajibu kwa mume kumtolea Zakaat-ul-Fitwr mkewe ambaye wana ugomvi mkubwa?


Swali: Ni wajibu kwa mume kumtolea Zakaat-ul-Fitwr mke wake ambaye wana ugomvi mkali?

Jibu: Zakaat-ul-Fitwr inamlazimu kila mtu kivyake na kila yule ambaye ni wajibu kumhudumikia ambapo miongoni mwa hao anaingia mke. Kwa sababu ni wajibu kwake kumhudumikia. Kukiwa kuna migogoro mikali baina yao basi kunatakiwa kuhukumiwe. Ikiwa kutahukumiwa kuwa mke ndiye muasi na hivyo hakuna uwajibu wa kumpa matumizi, basi katika hali hiyo kutakuwa hakuna uwajibu wa kumtolea Zakaat-ul-Fitwr kwa sababu ni yenye kufuata matumizi yake. Hivyo Zakaat-ul-Fitwr inaanguka kwa kuanguka matumizi yake.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/367-368)
  • Imechapishwa: 23/06/2017