Ni wajibu kwa mume kumhudumia mke kwa hali zote


Swali: Mwanamke akiwa ni mwalimu na ana mshahara wake itakuwa ni wajibu kwa mume kumpa matumizi au hapo itakuwa sio wajibu kwake?

Jibu: Ni wajibu kwa mume kumpa matumizi mke wake japokuwa atakuwa ni tajiri. Allaah (Ta´ala) amesema:

لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِ ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنفِقْ مِمَّا آتَاهُ اللَّـهُ

“Ili mwenye wasaa agharimu kutokana na wasaa wake na yule aliyebaniwa riziki yake, basi agharimie katika kile alichompa Allaah.” (65:07)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Riziki yao na mavazi yao ni wajibu kwenu kwa wema.”

Lakini hata hivyo inatakikana kwa mke, khaswa ikiwa mume wake ni fakiri na hakufunguliwa mali, basi amsaidie mahitajio ya nyumbani, familia na ya nafsi yake mwenyewe. Vinginevyo ni lazima kwa mume kumhudumia mke na watoto aliyezaa naye.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (38) http://binothaimeen.net/content/869
  • Imechapishwa: 01/07/2018