Ni wajibu kwa mtu kulipa swalah na swawm ya yale masiku yaliyompita pindi alipokuwa amezimia?

Swali: Kuna mwanamke alipatwa na kiharusi kabla ya Ramadhaan na hakupoteza fahami kikamilifu. Alikuwa anapoanza kuswali katikati ya swalah anaanza kuwazungumzisha walioko pembezoni naye. Ilipokaribia Ramadhaan ndipo akapoteza fahamu kikamilifu. Lakini madaktari wakasema kuwa anasikia. Kisha baada ya hapo akafariki katika Ramadhaan. Je, atolewe kafara?

Jibu: Mwanamke huyu ambaye alipatwa na kiharusi kabla ya Ramadhaan na akabaki na kitu katika fahamu na hisia anatakiwa kutolewa chakula kwa kila siku moja masikini. Kwa sababu maoni sahihi ni kwamba kuzirai hakumzuii mtu na kufunga. Kinachomzuia ni ule uwajibu wa swalah. Kwa mfano mtu akizirai siku mbili au tatu pasi na kutaka kwake hana uwajibu wa kulipa swala hizo. Ama ikiwa amezimia kwa kutaka kwake, kama kwa mfano amezimia kwa sababu ya bangi, basi ni lazima kulipa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/114)
  • Imechapishwa: 18/06/2017