Ni wajibu kwa mtu kukataza maovu kwa hali yoyote


Swali: Leo maovu yamekuwa mengi na ni wachache wanaokataza. Ni lipi la wajibu kwa waislamu juu ya hilo?

Jibu: Lililo la wajibu ni kukemea kwa kiasi cha uwezo wa mtu. Hivyo ndivyo alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule katika nyinyi atakayeona maovu, basi ayazuie kwa mkono wake. Asipoweza, afanye hivo kwa mdomo wake. Asipoweza, afanye hivo kwa moyo  wake – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”

Mtu akataze maovu kwa kiasi cha uwezo wake. Asiyakubali maovu kwa hali yoyote. Mtu anatakiwa kukataza maovu kwa kiasi cha uwezo wake; ima kwa mkono wake, mdomo wake au kwa moyo wake. Hii ndio ngazi ya mwisho. Asiridhie wala kuyakubali maovu. Hapana! Ayakataze maovu angalau kwa moyo wake. Akikataza maovu kwa moyo wake anatakiwa baada ya hapo ajitenge mbali na watu hao na ajitenge vilevile na sehemu hiyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (83) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-15-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 10/02/2018