Ni wajibu kwa kijana anayechelea uzinzi kuoa khasa akiwa na uwezo

Swali: Mimi ni kijana ambaye sijaoa. Ninapokaa peke yangu nafsi yangu inanizungumzisha haramu pamoja na kujua kwamba nina uwezo wa kuoa. Unaninasihi nini mimi na wengine mfano wangu?

Jibu: Ikiwa una uwezo wa kuoa basi ni lazima kwako kuharakisha na kutendea kazi maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Enyi kongamano la vijana! Yule ambaye katika nyinyi ana uwezo wa kuoa basi na aoe na yule asiyeweza basi na afunge – kwani hiyo ni ngao kwake.”

Ikiwa mtu anachelea kutumbukia katika machafu basi ni wajibu kwake kuoa ikiwa ni muweza. Ikiwa si muweza basi ni wajibu kwake kufunga ili kupunguza matamanio. Vilevile ukiwa huwezi na unapokaa peke yako ndio unafikiria mambo hayo, basi ni wajibu kwako kutokaa peke yako. Ishughulishe nafsi yako na kitu kitachokupa faida kama vile kusoma na kukaa na wengine ili usije kuingiliwa na fikira mbaya.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 19/10/2018