Swali: Baadhi ya maimamu katika swalah ya kusoma kwa sauti ya juu – kama swalah ya Maghrib, ´Ishaa na Fajr – baada ya kumaliza kusoma al-Faatihah wanakimbilia kusoma Suurah “al-Faatihah” na wala hawawaachii maimamu fursa waweze kusoma Suurah “al-Faatihah”. Unamnasihi nini yule imamu mwenye kufanya hivo? Kipi kinachomlazimu maamuma ikiwa hakusoma al-Faatihah katika zile Rak´ah mbili za mwanzo?

Jibu: Wale maimamu ambao wanafanya hivo na hawanyamazia baina ya kisomo cha al-Faatihah na Suurah ya baada yake, huenda kitendo hicho wanafanya kwa ujinga kama ambavyo huenda vilevile wanafanya hivo kwa ujuzi. Kuna uwezekano wakafanya hivo kwa ujuzi kwa sababu Hadiyth ya Samurah inayothibitisha minyamazo miwili – moja wapo ni baada ya kusoma al-Faatihah – wanachuoni wametofautiana juu ya usahihi wake. Wako ambao wameonelea kuwa ni Swahiyh na wakaitendea kazi na wakasema kuwa ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa imamu kunyamaza baada ya kusoma al-Faatihah. Mnyamazo uliopokelewa ni kwa njia isiyofungamana na haikuweka mpaka kama walivyouwekea mpaka baadhi ya Fuqahaa´ kwa kiwango cha maamuma kumaliza kusoma al-Faatihah. Bali ni kunyamaza kulikoachiwa ambako kunatenganisha ulazima wa kisomo [cha al-Faatihah] na naafilah yake. Wako wanachuoni wengine ambao wanaona kuwa Hadiyth hiyo si Swahiyh na pia wanaona kuwa inatakiwa kuunganisha kisomo. Hatuwezi kumkosoa yeyote vile ilivyompelekea elimu yake baada ya kutafiti na akafanya Ijtihaad. Lakini Hadiyth hiyo kwa mtazamo wangu ni hoja. Ameithibitisha Haafidhw Ibn Hajar katika “Fath-ul-Baariy” na akasema kwamba kunyamaza huku kumethibiti kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hili linahusiana na imamu.

Ama kuhusiana na maamuma wanatakiwa kusoma al-Faatihah japokuwa imamu atakuwa anasoma kutokana na yale maoni tunayoonelea. Hilo ni kutokana na kuenea kwa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hana swalah yule ambaye hakusoma mama wa Qur-aan.”

Hadiyth hii imethibiti katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy, Muslim na vitabu vyenginevyo.

Katika Hadiyth ya ´Ubaadah bin as-Swaamit iliopokelewa na waandishi wa “as-Sunan” ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalisha swalah ya “al-Fajr” na alipomaliza akasema:

“Huenda nyinyi mnasoma nyuma ya imamu wenu?” Wakaitikia: “Ndio.” Akasema: “Msifanye hivo isipokuwa tu mama wa Qur-aan. Kwani hana Qur-aan yule asiyeisoma.”

Hili ni dhahiri kwamba imamu pia anatakiwa kusoma hata katika swalah ya kusoma kwa sauti. Kwa sababu hii ni swalah ya al-Fajr nayo ni swalah ambayo mtu anasoma kwa sauti ya juu. Hadiyth hii inaonyesha wazi kwamba mswaliji anatakiwa kusoma hata kama imamu pia anasoma. Inatiwa nguvu na ueneaji wa Hadiyth iliotangulia ambayo tumeashiria. Kwa ajili hii tunasema kumwambia maamuma: soma al-Faatihah. Ikiwa utaimaliza kabla imamu hajaanza kisomo kingine baada yake ni vizuri. Imamu akianza kusoma Suurah nyingine baada yake kabla ya wewe kumaliza kusoma Suurah “al-Faatihah” basi endelea mpaka uimalize.

Swali: Ni ngumu mswaliji kusoma al-Faatihah na wakati huohuo imamu anasoma. Jambo hilo linaweza kuleta mchanganyiko katika kisomo na matokeo yake kisomo kikawa si sahihi. Kwa sababu mswaliji huyu anasoma kwa sauti ya kimyakimya na huku imamu anasoma kwa sauti ya juu.

Jibu: Nataraji maneno yako ugumu unamaanisha kwa baadhi na si kwamba unamaanisha aina ya jambo hili ni ngumu. Kama ulivosema inaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya watu kusoma na huku imamu pia anasoma. Lakini kwa watu wengine si gumu. Hili ni jambo tumelijaribu. Mtu anaweza kusoma na huku imamu pia anasoma, hili ni jambo tumelijaribu.

Swali: Kuhusu yule ambaye ni ngumu kwake.

Jibu: Anatakiwa ajaribu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (01) http://binothaimeen.net/content/6632
  • Imechapishwa: 07/02/2019