Ni wajibu kwa baba kumhijisha mtoto wake?

Swali: Mimi ni mwanafunzi ambaye nataka kuhiji. Je, nichukue pesa kutoka kwa baba yangu au nisubiri mpaka pale nitapoajiriwa na nikawa na uwezo wa kwenda hajj? Ni lipi bora kwangu?

Jibu: Ni jambo linalojulikana kwamba mwanafunzi ambaye hana pesa haimlazimu kumuomba baba yake pesa ya kuhiji nayo. Kwa sababu hajj haijakuwa wajibu kwake. Lakini baba yake mwenyewe akiona mpe pesa za kuhiji nazo kwa ajili ya kumtendea wema – na sio kwamba ni wajibu kwa baba kufanya hivo – ni sawa. Kufanya hivi ni katika kusaidiana katika wema na uchaji na ni katika kuunga udugu vilevile.

Kwa hivyo nawashauri kina baba wote ambao wako na uwezo wawasaidie watoto wao katika kuhiji japokuwa sio lazima kwao kufanya hivo. Kwa sababu kufanya hivi ni katika wema na vilevile ni katika kuunga udugu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (63) http://binothaimeen.net/content/1432
  • Imechapishwa: 26/12/2019