Ni wajibu kuwafunza ´Awwaam kuwa Allaah yuko juu

Swali: Baadhi ya watu ukiwauliza “Allaah Yuko wapi?” Wanasema “Kila mahali”. Hawajui kama Allaah Yuko juu mbinguni Amelingana juu ya ´Arshi.

Jibu: Jibu ni kama alivosema mjakazi wakati Mtume (´alayhis-Salaam) alipoulizwa “Allaah Yuko wapi?” Akasema “Mbinguni”. Kadhalika hilo ni kwa andiko la Qur-aan.

Swali: Atuhumiwe mwenye kusema kuwa Allaah Yuko kila mahali?

Jibu: Afundishwe.

Swali: Asituhumiwe juu ya ´Aqiydah yake?

Jibu: Ikiwa ni mtu ambaye sio msomi afunzwe. Huu ni munkari. Ni kufuru. Hivyo afunzwe kuwa Allaah Yuko juu ya ´Arshi mbinguni:

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ

”Je, mnadhani mko [katika] amani na Aliyeko mbinguni [juu].” (67:16)

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa Rahmah amelingana juu ya ´Arshi.” (20:05)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah (02)
  • Imechapishwa: 09/08/2020