Swali: Mimi nilikuwa na Jamaa´at-ut-Tabliygh. Namna muda ulivyokuwa unaenda nikaona namna mfumo wao ulivyo na Bid´ah na Taswawwuf. Nilikuwa nao karibu miaka tano. Inajuzu kwangu kutahadharisha nao na khaswa kwa kuzingatia ya kwamba ndugu zetu wa kisaudi wana mawasiliano na wao?

Jibu: Hapa Saudi Arabia tuna Da´wah. Tuna wizara ya kipekee kwa ajili ya Da´wah. Humo mna wanachuoni. Tuko katika njia iliyonyooka. ´Aqiydah yetu ni ya Tawhiyd. Hatuna haja ya kuingiza Da´wah zisizojulikana na wala hatujui zimetokea wapi. Maadamu umeyajua haya na umeijua hali ya Jamaa´at-ut-Tabliygh, ni wajibu kwako kutahadharisha nao. Haifai kwako kunyamaza ilihali unajua ni makosa yepi walonayo. Ni wajibu kwako kutahadharisha nao. Huku ni kuwatakia kheri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Dini ni kupeana nasaha.” Tukasema: “Kwa nani, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Kwa ajili ya Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake, viongozi wa waislamu na watu wa kawaida.”

Tunaishi katika nchi ya Tawhiyd na ya Da´wah. Tuna wizara iliyotengwa khaswa kwa ajili ya Da´wah na maelekezo. Vipi watakuja katika nchi yetu na kulingania kwa Allaah na kuivamia nchi yetu, watoto wetu, miji yetu na vijiji vyetu? Haijuzu kuwaachia fursa ya kufanya hivo. Ni wajibu kwa wale walinganizi wa kimataifa na wenye upeo wasambae katika nchi hii na wasiwape nafasi wengine katika wale wanaotujia kutoka nje.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=BOkVhc2UBuQ
  • Imechapishwa: 14/01/2017