Ni Wajibu Kutahadharisha ISIS Na Ahl-ul-Bid´ah Wengine


Swali: Unaweza kuwatahadharisha waislamu juu ya ukhatari wa ISIS na kuwahimiza watu kujiepusha nao na kutowa na huruma kwao?
Jibu: Ni wajibu kutahadharisha kila kundi potevu lenye kwenda kinyume na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ni wajibu kuwafunza watu mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Baadhi ya watu hawajui mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ndio maana hufikiria kuwa kila mtu yuko katika haki na hawatofautishi kati ya mtu wa Bid´ah na Sunniy. Ni wajibu kwa mtu kujifunza mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na kuuliza juu yake ili aweze kushikamana nao na kuufuata.

Ni wajibu kushikamana na mkusanyiko wa waislamu na kiongozi wao na khaswa wakati wa vurugu. Mtu anatakiwa kushikamana na mkusanyiko na kmusikiliza na kumtii mtawala. Hii ndio njia sahihi na ya uokozi. Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Watu walikimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya mambo ya kheri lakini mimi nikimuuliza mambo ya shari nikichelea nisitumbukie ndani yake. Nikasema: “Mtume wa Allaa! Tulikuwa katika mambo ya ujinga na shari ambapo akatuokoa Allaah kwa kutuletea kheri hii ya Uislamu. Je, baada ya kheri hii itakuja shari?” Akasema: “Ndiyo.” Nikasema “Je, baada ya shari hiyo itakuja kheri?” Akasema: “Ndio, lakini ina moshi.” Nikamuuliza: “Ni upi moshi wake?” Akasema: “Ni watu wanafuata mwenendo ambao sio mwenendo wangu mimi na wanaongoza bila kufuata mwongozo wangu mimi. Kuna mambo utakubaliana nao lakini mengine hutoyakubali.” Nikasema: “Je, baada ya kheri hiyo kutakuwa na shari?” Akasema: “Ndiyo, watu wanawaita watu hali yakuwa wamesimama katika milango ya Motoni. Atakayewafuata wanamtupa Motoni.” Nikasema: “Mtume akasema! Tupe sifa zao watu hao.” Akasema: “Ni watu kama sisi na wanatamka kwa maneno yetu.” Nikasema: “Unanishauri nini ikiinikuta hali hiyo?” Akasema: “Jilazimishe kuwa katika mkusanyiko wa waislamu na kiongozi wao.” Nikasema: “Ikiwa hakuna mkusanyiko wa waislamu wala kiongozi.” Akasema: “Jiepushe na makundi hayo yote hata kama utahitajia kung´ata meno shina la mti mpaka ufe.” al-Bukhaariy (3606) na Muslim (1847).

Usiwe na wapotevu na Ahl-ul-Bid´ah waliopinda. Usiwe na wao kamwe! Jiepushe nao. Kuwa pamoja na kiongozi na mkusanyiko wa waislamu. Ikiwa waislamu hawana mkusanyiko wala kiongozo basi yaepuke mapote yote na ubaki mwenyewe katika Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=153335 Tarehe: 1436-09-17/2015-07-04
  • Imechapishwa: 06/11/2016