Ni wajibu kumtazama mwanamke kabla ya kumuoa? Kunatazamwa nini?


Swali: Kijana anapotaka kumposa mmoja katika wasichana. Katika hali hii, je ni wajibu kwake (kijana huyo) kumuona? Na je, ni sawa msichana huyo kufunua kichwa chake ili abainishe uzuri wake zaidi kwa mposaji wake?

Jibu: Hakuna ubaya, lakini sio wajibu bali ni jambo limependekezwa. Ni jambo limependekezwa (kijana huyo) akamuona na yeye (msichana huyo) akamuona (mvulana huyo). Kwa kuwa hii ni njia ya karibu ya kukubali. Mtume (´alayhis-Salaam) kamwamrisha mwenye kutaka kuchumbia atazame (kwanza). Akifunua uso wake, na miguu yake na kichwa chake, haina neno kutokana na kauli ya sahihi. Wamesema baadhi ya wanachuoni kuwa inatosha uso wake na vitanga vyake, lakini kauli ya sahihi ni kuwa haina neno kufunua kichwa na miguu atazame apendekezwe na uzuri wake. Wanaweza kutazamana (kwa kuwepo walii wa mwanamke)kwa kuwa hii ni njia ya karibu ya kuweza kukubali. Hili liwe pasina mchanganyiko (yaani wasiwe wao wawili tu), bali wawe pamoja na baba yake na msichana, au kaka yake au mwanamke mwingine. Wasichanganyike wao wawili tu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb (770)
  • Imechapishwa: 15/03/2018