Ni wajibu kuhama kutoka nchi ya kikafiri na kwenda ya Kiislamu?

Swali: Ni wajibu kuhajiri kutoka katika mji wa kikafiri na kwenda katika mji wa Kiislamu?

Jibu: Ni wajibu ikiwa kama yuko na uwezo. Haijuzu kwake kueshi kati ya makafiri ilihali yuko na uwezo. Katika hali hiyo anaingia ndani ya matishio:

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖوَسَاءَتْ مَصِيرًا إِلَّا الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلً فَأُولَـٰئِكَ عَسَى اللَّـهُ أَن يَعْفُوَ عَنْهُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَفُوًّا غَفُورًا

“Hakika wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamejidhulumu nafsi zao, watawaambia: “Mlikuwa katika hali gani?” Watasema: “Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.” Watasema: “Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa ya wasaa mkahajiri?” Basi hao makazi yao yatakuwa ni [Moto wa] Jahannam – na uovu ulioje mahali pa kuishia. Isipokuwa wale waliokandamizwa kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao hawakuweza kupata hila yoyote wala hawawezi kuongoza njia. Basi hao huenda Allaah Akawasamehe. Na Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kughufuria.” (04:97-99)

Aayah hii inawahusu wale ambao hawakuhajiri ilihali walikuwa na uwezo wa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdah–14340316.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020