Ni wachache wanaorekebisha ´Aqiydah


Kuna wanachuoni wengi lakini ni wachache ambao huchagua mwelekeo huu ambao ni kurekebisha ´Aqiydah. Ni wachache lakini  ukweli wa mambo wao ndio matunda ya wanachuoni katika kila zama na pahali. Wao ndio wenye kuihuisha dini hii na kuilinda ´Aqiydah kutokamana na hoja tata na fikira mbaya. Haya ni katika fadhilah za Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) na ni usadikisho wa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakutoacha kuwepo katika Ummah wangu wenye kushikamana hali ya kuwa ni wenye kushinda. Hawatodhurika na wale wenye kuwakosesha nusura na wenye kwenda kinyume nao mpaka ifike amri ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) nao wako katika hayo.”

Imamu huyu (Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab) alilingania katika dini ya Allaah na kusahihisha ´Aqiydah. Aliandika vitabu na vijitabu. Aliwafundisha wanafunzi na wanafunzi wakahajiri kwenda kwake kutoka katika miji mbalimbali.

  • Mhusika: Imâm Sâlih bin Fawzân al-Fawzân
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/02011436.mp3 Muhadhara: Haqiyqatu Da´wat-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Imechapishwa: 19/03/2021