Ni vitabu vipi bora inapokuja katika Siyrah?

Swali: Ni kitabu kipi bora inapokuja katika Siyrah?

Jibu: Siyrah ya Ibn Hishaam ni miongoni mwa vitabu bora vilivyoandikwa katika maudhui haya na “al-Bidaayah wan-Nihaayah” ya Ibn Kathiyr. Shaykh na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab ametunga kitabu “Mukhtaswar-us-Siyrah”. Vivyo hivyo mwanae ´Abdullaah ana vitabu viwili vifupi vizuri ambapo ndani yake amebainisha ´Aqiydah, kunyofoa hukumu kutoka katika Siyrah na yale yanayojulisha Tawhiyd.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 12/11/2021