Ni vipi mwanadamu atakuwa ni mwenye kubeba jukumu?

Swali: Ni vipi mtu atabeba jukumu/amana ilihali amekalifishwa na hakupewa chaguo katika jukumu hilo?

Jibu: Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَحَمَلَهَا الْإِنسَانُ

“… lakini akaibeba mtu.”[1]

Allaah (´Azza wa Jall) hamdhulumu yeyote. Lau mtu asingelichagua jukumu hili akalibeba basi  asingelisema:

وَحَمَلَهَا الْإِنسَانُ

“… lakini akaibeba mtu.”

Kama tulivyotaja katika tafsiri ya kwamba mtu amebeba majukumu hayo kutokana na ile akili ambayo Allaah amempa, kuyaendesha mambo, Mitume aliotumiliziwa na akateremshiwa Vitabu. Ni kama kwamba amesema kwamba yeye ndiye mwenye kuistahiki na kwamba atayabeba kwa sababu yeye ndiye yuko na Qur-aan, Sunnah, akili na uwezo wa kuyapambanua mambo.

[1] 33:72

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (77) http://binothaimeen.net/content/1761
  • Imechapishwa: 21/09/2020