Ni vipi mtu atamnuia Allaah katika kusoma elimu?

Swali: Inasemekana kwamba ni lazima kuwa na nia nzuri wakati wa kujifunza elimu. Vipi inakuwa hivo?

Jibu: Ni lazima na nia nzuri. Kwa sababu kujifunza elimu ni miongoni mwa faradhi zilizo bora na tukufu zaidi. Ni ´ibaadah na ´ibaadah ni lazima kumtakasia Allaah nia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika kila kitendo kinategemea nia.”

Mwenye kuswali kwa ajili ya mwengine asiyekuwa Allaah swalah yake ni batili. Mwenye kujifunza elimu kwa ajili ya mwengine asiyekuwa Allaah juu yake kuna makemeo makali.

Makusudio ya kuwa kumnuia Allaah ni mtu anuie kwa kusoma kwake uso wa Allaah na Nyumba ya Peponi na aiokoe nafsi yake na nafsi za wengine kutokamana na ujinga. Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:

“Anuie kuondosha ujinga kutoka katika nafsi yake na kutoka kwa wengine.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=audioinfo&audioid=191634
  • Imechapishwa: 19/04/2020