Ni vipi inaswaliwa Maghrib ikiwa ni swalah ya khofu?


Swali: Ni vipi inakuwa swalah ya khofu (صلاة الخوف) ikiwa ni Maghrib?

Jibu: Kundi la kwanza linaswali zile Rak´ah mbili za mwanzo. Kisha liswali Rak´ah moja kivyake na huku imamu bado amesimama. Kisha kuje kundi la pili na liswali Rak´ah moja na imamu. Halafu imame abaki amekaa na huku kundi hilo liswali Rak´ah mbili zilizobaki na wakamilishe Maghrib.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (12) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-19-10-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 17/09/2017