Ni vipi anatoa kafara aliyeshindwa kufunga kwa sababu ya utuuzima?

Swali: Kuna mwanamke mtumzima anashtakia juu ya maradhi na kwamba hawezi kufunga. Ni vipi atakabiliana na hilo? Je, atoe kila siku Swaa´ (pishi) au atoe mara moja mwishoni mwa Ramadhaan?

Jibu: Ana khiyari; akitaka atatoa fidia ya kila siku kwa siku. Lakini fidia ya siku ya pili asimpe yule fakiri wa kwanza. Kwa kuwa ni lazima idadi ya mafukara iwe sawa na idadi ya masiku. Ikiwa mwezi una siku thelathini basi idadi ya masikini au mafukara inakuwa thelathini na ikiwa ni siku ishirini na tisa basi idadi ya mafukara inakuwa ishirini na tisa.

Kuhusu kiwango anachotakiwa kutoa sio kama alivosema muulizaji kwamba ni Swaa´. Sio Swaa´, bali ni chini ya hapo. Kiwango cha Swaa´ tuichonacho kinawatosha mafukara tano.

Inajuzu kwa mtu baada ya siku kumi akawakusanya mafukara kumi na akawalisha. Baada ya siku zengine kumi akawakusanya mafukara wengine kumi – mbali na wale wa mwanzo – akawalisha. Baada ya kumi lingine akawakusanya mafukara wengine kumi – mbali na wale wa mwanzo – akawalisha. Inafaa vilevile katika ile siku ya mwisho akawakusanya mafukara thelathini kama, ambavyo alikuwa akifanya Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) wakati alipokuwa mtumzima.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1508
  • Imechapishwa: 13/06/2018