Ni usiku unakuweko kila mwaka

Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

سَلَامٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ

“Ni amani mpaka kuchomoza alfajiri!”[1]

Bi maana usiku huo unaanza pale jua linapozama na mpaka kupambazuka kwa alfajiri. Kumepokelewa Hadiyth nyingi juu ya ubora wake na kwamba unakuwa katika Ramadhaan na katika zile nyusiku zake kumi za mwisho na inakuwa katika zile nyusiku za witiri. Usiku huo ni wenye kuendelea kila mwaka mpaka kisimame Qiyaamah. Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya I´tikaaf na akifanya ´ibaadah kwa wingi katika zile siku kumi za mwisho za Ramadhaan kwa kutaraji usiku wa Qadr.

[1] 97:05

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, uk. 1098
  • Imechapishwa: 16/05/2020