Ni sawa kusema kafiri fulani yuko Motoni?

Swali: Ni ipi hukumu ya yule mwenye kumhukumu kafiri kwa dhati yake baada ya kufa kwake ya kwamba yuko Motoni? Je, akatazwe kufanya hivo?

Jibu: Kumhukumu kafiri ambaye anakufa katika ukafiri wa asili endapo makusudio itakuwa ni kwamba anaingia katika jumla ya makafiri pasi na kumkatia mtu kwa dhati yake ni sawa. Ama kumkatia mafikio yake kafiri kwa dhati yake na jina lake haifai isipokuwa tu yule ambaye kumethibiti juu yake dalili ya Kishari´ah. Kama mfano wa Fir´awn na Abu Lahab.

Hapana shaka juu ya mafikio ya yule kafiri wa asili. Lakini hakuna yeyote awezaye kusema kwa kukata ni hali ipi aliokufa nayo katika kile kipindi cha mwisho. Hakuna yeyote anayejua hayo isipokuwa Allaah pekee.

Kafiri huyu ambaye anahukumiwa na baadhi ya watu ya kwamba ni katika watu wa Motoni anaweza kuwa anaingia katika Ahl-ul-Fatrah ambao watapewa mtihani huko Aakhirah. Kwa kuzingatia ya kwamba kafiri ambaye Shari´ah inamhukumu Moto ni yule kafiri wa asili ambaye hashuhudii ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Kwa msemo mwingine ni yule asiyekuwa muislamu. Haingii katika watu hao muislamu ambaye ametumbukia katika kufuru usiopelekea katika kuritadi. Kwa sababu mambo mengi yenye kukufurisha ambayo baadhi ya waislamu wanatumbukia ndani yake hayawatoi katika Uislamu. Mengi katika mambo hayo yanaingia katika madhambi makubwa ambayo hayapelei mtu kudumishwa Motoni milele.

  • Mhusika: Shaykh Naaswir bin ´Abdil-Kariym al-´Aql
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://ar.islamway.net/fatwa/33577/%D8%A7%D9%84%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D8%A7%D9%84%D9%83%D8%A7%D9%81%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B9%D9%8A%D9%86-%D8%A8%D8%A3%D9%86%D9%87-%D9%85%D9%86-%D8%A3%D9%87%D9%84-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%A7%D8%B1
  • Imechapishwa: 25/07/2017