Swali: Ni sahihi ya kwamba hakuna kukatazana katika mambo yalio na tofauti?

Jibu: Kwanza ikiwa ni katika ´Aqiydah itambulike kuwa hakuna tofauti katika ´Aqiydah. Lililo la wajibu kwetu ni kufuata mdhehebu ya Salaf na tusiwe na tofauti. Mambo ya tofauti ikiwa yanahusiana na mambo ya Fiqh, yamegawanyika sehemu mbili:

1- Mambo ambayo dalili zimedhihirika katika moja ya kauli mbili. Ni wajibu kumzindua mwenye kwenda kinyume kwa kuwa dalili iko na yule mwingine. Inatakiwa kumuwekea wazi hili.

2- Ikiwa dalili haikudhihirika na kauli zote mbili zina nguvu, kuna uwezekano ikawa hivi na kuna uwezekano ikawa vile, wote wawili wawili hawakudhihirikiwa na dalili, hakuna kukemeana katika mambo ya Ijtihaad.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_07.mp3
  • Imechapishwa: 27/06/2018