Ni Sahihi Kuwatahadharisha


Swali: Nimesoma kitabu chenu ”al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah”. Katika maelezo ya chini nimeona namna walinganizi wanavyotajwa kama vile Sayyid Qutwub, al-Mawduudiy, Salmaan al-´Awdah, Naaswir al-´Umar na ´Aa´idh al-Qarniy.

al-Fawzaan: Maelezo ya chini sio yangu. Ni maelezo yake.

Muulizaji: Ni maelezo ya Shaykh Jamaal.

al-Fawzaan: Ndio.

Muulizaji: Kuna wanaosema kuwa maelezo hayo ya chini yameandikwa baada ya wewe kuandika utangulizi wako. Je, ni kweli?

Jibu: Hapana. Alikusanya maelezo hayo na akayaongeza kwenye kitabu.

Swali: Maelezo hayo unayatambua?

Jibu: Ndio. Maelezo hayo yana nini?

Muulizaji: Baadhi wanasema kuwa Shaykh Jamaal aliyaongeza baada ya kukuonyesha kitabu hicho.

al-Fawzaan: Ndio, yana nini?

Swali: Kutahadharishwa kwa walinganizi hao ni sahihi?

Jibu: Ndio, ni sahihi[1].

[1] Imaam Swaalih al-Fawzaan amesema: Himdi zote anastahiki Allaah. Nimempa idhini Shaykh Jamaal bin Furayhaan al-Haarithiy ya kuchapisha kwa mara nyingine kitabu “al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah” ambaye amekusanya majibu yangu ya maswali ya wanafunzi kupitia mikutano na durusi. Nimempa idhini ya kuchapisha kitabu pamoja na taaliki zake na nyongeza zingine ambazo hazikuwepo katika machapisho yaliyotangulia. Allaah Awaongoze [watu] wote katika haki na kuitendea kazi. Swalah na salaam zimwendee Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.”

Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

1423-12-23 (al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 13)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=y-61KUhRXwU
  • Imechapishwa: 08/04/2017