Ni nini Tahniyk na ni jambo maalum kwa Mtume peke yake?

Swali: Nini Tahniyk (التحنيك)? Ni ipi hukumu ya kufanya hivo? Je, ni jambo linalomuhusu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake?

Jibu: Tahniyk ni kuweka tende kwenye koo ya mtoto mchanga. Sio jambo maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake. Lakini anaweza kumfanya hivo baba yake, mama yake au mtu mwingine yeyote ili iwe kitu cha kwanza kitachoingia kooni mwake ni utamtam. Namna inavyotakiwa kufanywa kwanza aisagesage tende ile kisha aiingize kinywani mwa mtoto.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 27/10/2018