Swali: Ni yapi makusudio ya kuziwekea Ta´wiyl sifa na Ash´ariyyah ndio walioziwekea Ta´wiyl sifa?

Jibu: Kuziwekea Ta´wiyl sifa makudio yake ni kuzifasiri kinyume na tafsiri yake sahihi. Hii ndio inaitwa Ta´wiyl. Kuzifasiri kinyume na tafsiri yake sahihi na kuzitoa katika ile maana yake iliyoonyesha.

Ashaa´irah ni katika makundi yaliyowekea Ta´wiyl sifa. Jahmiyyah, Mu´tazilah, Ashaa´irah na Maaturiydiyyah, wote hawa wameziwekea sifa Ta´wiyl.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (21) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-2-22.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020