Swali: Nilimuona mtu katika Twawaaf akiwa na hirizi. Nikamnasihi aivue akakataa, matokeo yake nikawa nimeiondosha kwa nguvu. Je, kitendo changu ni sahihi?

Jibu: Kuna nini ndani yake? Qur-aan au shirki? Ikiwa kumeandikwa Qur-aan, wanachuoni wametofautiana juu ya suala hili. Na kama ina shirki, ni ya kishirki. Mnasihi aivue. Asipofanya hivo mpelekee suala hili ambaye ana mamlaka atamvua nayo. Ama wewe kumvua nayo hili litaleta shari na fitina. Huenda akakupiga, huenda akakulipiza kisasi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule katika nyinyi mwenye kuona maovu ayaondoshe kwa mkono wake.”

Hili linahusiana kama uko na mamlaka.

“Asipoweza, afanye hivo kwa ulimi wake.”

Inatosheleza kumpa nasaha, mawaidha na ubainifu.

“Asipoweza, afanye hivo kwa moyo wake.”

Mtawala na manaibu wa mtawala ndio wanaoweza kubadilisha kwa mkono.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathulmajid%207%20-%20… Toleo la: 22.05.2015
  • Imechapishwa: 11/02/2017