Ni nani anatakiwa kuwafunza wanawake?

Kipindi cha mwisho imekuwa ni jambo la kawaida hapa Dameski kwa wanawake kwenda misikitini katika nyakati maalum kwa ajili ya kusikiliza darsa inayotolewa na mwanamke. Kwa madai yao eti wanawaita wanawake hawa ”walinganizi wa kike” (الداعيات). Hilo ni jambo lililozuliwa ambalo halikuwa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala katika wakati wa wema waliotangulia. Wanachuoni wema ndio wanaotakiwa kuwafunza wanawake sehemu maalum, kama ilivyo katika Hadiyth hii, au msikitini pamoja na wanaume, wakiwa ni wenye kutengana na wanaume ikiwa jambo hilo litawezekana. Vinginevyo watashindwa na wanaume na hawatoweza kujifunza wala kuuliza.

Hii leo kukipatikana mwanamke ambaye ana kitu katika elimu na uelewa uliochukuliwa kutoka katika Qur-aan na Sunnah, basi hakuna neno akawa na kikao maalum nyumbani kwake au katika nyumba ya mmoja wao. Hilo ni kheri kwao. Ni vipi isiwe hivyo ilihali Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu swalah ya mkusanyiko ya wanawake msikitini:

”Msiwazuie vijakazi wa Allaah kutokamana na misikiti ya Allaah. Nyumbani zao ni bora kwao.”?

Jambo likiwa hivi juu ya swalah ambayo ni lazima kwa mwanamke wa Kiislamu kulazimiana na adabu na heshima zaidi kuliko anavofanya kwenginepo, ni vipi basi elimu isiwe kwenye majumba? Hili khaswa kwa kuzingatia ya kwamba baadhi yao ni wenye kunyanyua sauti zao msikitini mpaka zikawa mbaya na zenye kusemwa vibaya. Kwa masikitiko makubwa haya tumeyashuhudiana wenyewe na kuyaona.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (6/1/401)
  • Imechapishwa: 16/05/2019