Ni nani ambaye ana haki zaidi ya kupewa zakaah katika yale mafungu manne?

Swali: Je, mtu anatakiwa kuanza kimpangilio yale mafungu manane kama alivyotaja Allaah (´Azza wa Jall)?

Jibu: Wenye haki zaidi ni mafukara. Mola (´Azza wa Jall) ameanza kuwataja wao. Wanafuatia ni masikini. Kwa sababu masikini ni wale ambao wanaweza kupata baadhi ya vitu na mafukara wanakuwa ni wahitaji zaidi.

Mwenye kuifanyia kazi (العامل عليها) ni wale wafanyakazi ambao wanaagizwa na mtawala kuichukua kutoka kwa watu. Kile wanachokichukua inakuwa ndio ni malipo yao.

Wale ambao zinalainishwa nyoyo zao zinatofautiana hali zao; huenda haja yao ikawa kubwa na huenda haja yao isiwe kubwa.

Kwa hivyo muumini anatakiwa kuwa makini zaidi ampe yule ambaye ni muhitaji zaidi kisha ambaye anafuatia kwa haja na ampe ambaye anafaa zaidi kisha anafuatia kwa kufaa zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21622/من-الاولى-بالبدء-في-اصناف-الزكاة-والصدقة
  • Imechapishwa: 03/09/2022