Ni nani aliyesema mtawala anasihiwe hadharani?

Swali: Vipi tutajumuisha kati ya kauli ya baadhi ya wanachuoni kwamba mtawala akikosea hadharani akatazwe hadharani na kati ya Hadiyth…

Jibu: Ni nani aliyesema hivi? Hakuna mwanachuoni aliyesema hivi. Hili limesemwa na anayejifanya kuwa ni mwanachuoni au mtu mjinga. Hakatazwi hadharani na wala haijuzu kumkataza hadharani. Anasihiwe kwa siri. Hili ndilo limethibiti katika Hadiyth:

“… amshike mkono na amnasihi. Akikubali, la sivyo atakuwa ametekeleza dhimma yake.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (70) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13905
  • Imechapishwa: 16/11/2014