Hoja na dalili kutoka katika Kitabu cha Allaah, Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), maneno ya Salaf wenye kuzingatiwa na maimamu wa uongofu, yote yanabainisha na kuafikiana juu ya kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah na hayakuumbwa na mwenye kusema Qur-aan imeumbwa ni kafiri. Kwa kuwa amekadhibisha Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah na ameenda kinyume na maafikiano ya Salaf – Allaah awawie radhi. Maswahabah wamekubaliana juu ya kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah na kadhalika Taabi´uun, mpaka alipokuwa khabithi huyu Jahm bin Swafwaan akamzulia Allaah uongo huu mkubwa kwamba Qur-aan imeumbwa kama ambavyo vilevile alivyozusha uongo wa kuzikanusha sifa za Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) na kuzipotosha. Hivyo akawa amekanusha kuwepo juu kwa Allaah (al-´Uluw), juu ya mbingu, akakanusha kuwa amelingana juu ya ´Arshi, akakanusha kuwa Allaah anazungumza, akakanusha kwamba Ibraahiym ni Khaliyl wa Allaah, Muusa ni msemezwa wa Allaah na upotevu mwingineo.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaasid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/343)
  • Imechapishwa: 19/05/2015