Ni mnyama yupi katika Udhhiyah bora kumchinja?


Swali: Mwaka ulopita nilitaka kuchinja ng´ombe nikaambiwa kwamba kondoo ndio bora. Je, kumethibiti Hadiyth zinazoonesha kwamba kondoo ndio bora zaidi?

Jibu: Ndio. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichinja kondoo mbili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akichinja kondoo na mbuzi. Ikiwa ni wepesi kwake kuchinja kondo au mbuzi ndio bora. Akichinja vilevile ng´ombe au ngamia hakuna neno. Maswahabah walifanya yote mawili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pia alichinja ng´ombe na ngamia katika hajj ya kuaga kwa ajili ya kujitolea. Kwa hiyo mtu akichinja ngamia au ng´ombe hakuna neno. Lakini kondoo na mbuzi ndio bora kukiwa kuna wepesi wa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/12102/%D8%AA%D9%81%D8%B6%D9%8A%D9%84-%D8%A7%D8%B6%D8%AD%D9%8A%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%83%D8%A8%D8%B4-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D8%A7%D9%84%D8%A8%D9%82%D8%B1%D8%A9-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%A8%D9%84
  • Imechapishwa: 17/08/2018