Ni lipi bora kwa anayeingia mskitini akawakuta watu wanaswali Tarawiyh?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali mkusanyiko wa pili na huku watu wanaswali swalah ya Tarawiyh katika Ramadhaan? Kwa kuwa nimewasikia baadhi ya watu wakisema kuwa ni Bid´ah na wengine wakisema kuwa katika yale masiku kumi [ya mwisho] hakuna neno ama katika masiku mengine ni Bid´ah sawa iwe katika yale masiku ya Ramadhaan ya mwanzo au ya katikati.

Jibu: Sahihi inapokuja katika haya ni kwamba ikiwa mtu ataingia, sawa awe peke yake au wako wengi, na wakawakuta watu wanaswali swalah ya Tarawiyh basi wanatakiwa kujiunga na imamu kwa nia ya kwamba wanaswali ´Ishaa. Pindi imamu ataleta Tasliym basi watakamilisha zile Rak´ah zilizobaki za ´Ishaa ambapo kila mmoja atakamilisha kivyake na si kwa pamoja. Haya ndio maoni ya sawa.

Ama kuswali swalah za mikusanyiko mbili katika msikiti mmoja hili pasi na shaka ni jambo ambalo halikuwekwa katika Shari´ah. Lakini tunamwambia ajiunge na imamu kwa njia ya ´Ishaa.

Iwapo muulizaji atauliza kama inasihi kwa mwenye kuswali swalah ya faradhi kuongozwa na anayeswali swalah ya Sunnah? Jibu ni kwamba inasihi. Hili ni jambo limetokea wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakika Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akiswali pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) swalah ya ´Ishaa kisha anaenda kwa watu wake na anawaswalisha swalah hiyohiyo. Kwa haki yake ni Sunnah na kwa haki ya wale wengine ni faradhi. Haya yalitokea wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo Allaah (´Azza wa Jall) akamkubalia hilo. Bali udhahiri wa mambo ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa analijua hilo na yeye pia akamkubalia. Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema ya kwamba iwapo mtu ataingia na akawakuta watu wanaswali Tarawiyh basi ajiunge nao kwa kunuia ´Ishaa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (32) http://binothaimeen.net/content/718
  • Imechapishwa: 10/11/2017