Ni lini Tabarruk inakuwa shirki kubwa au ndogo?

Swali: Ni lini Tabarruk inakuwa shirki na lini inakuwa si shirki?

Jibu: Pale atapoamini kwamba baraka ni zenye kutoka kwa asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jall). Akifanya Tabarruk kwenye jiwe au mti na akaamini kuwa kitu hichi ndio chenye kutunuku baraka, katika hali hii inakuwa shirki kubwa. Lakini akiamini kuwa kitu hichi ni sababu tu ya baraka na baraka ni yenye kutoka kwa Allaah na kitu hichi ni sababu inayofanya kupatikana kwa baraka, hii ni shirki ndogo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 56
  • Imechapishwa: 08/07/2018