Ni lini nalipa sunnah ya Fajr pindi inapompita mtu?

Swali: Ni lini nalipa sunnah ya Fajr pindi inaponipita?

Jibu: Mtu anapokosa Sunnah ya Fajr basi muislamu wa kiume na muislamu wa kike amepewa khiyari; akitaka ataiswali baada ya swalah na akitaka ataiswali baada ya kuchomoza jua na ndio bora zaidi. Yote hayo yamepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imepokelewa kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa alimuona mwenye kuswali baada ya swalah ya Fajr ambapo akamkemea na mtu yule akasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Ni Sunnah ya Fajr” ambapo akamnyamazia. Vivyo hivyo imekuja kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amri ya kuilipa baada ya kuchomoza kwa jua. Yote hayo – kwa himdi za Allaah – yanafaa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/374)
  • Imechapishwa: 16/08/2022