Ni lini mtoto anawajibika kufunga na kuswali?

Swali: Ni lini mtoto anawajibika kufunga? Ni mpaka wa miaka mingapi ambayo anawajibika kufunga?

Jibu: Mtoto anaamrishwa kuswali anapofikisha miaka saba na anapigwa kwayo anapofikisha miaka kumi. Swalah hiyo itakuwa ni wajibu pindi atapobaleghe. Kubaleghe kunaptikana kwa moja ya mambo yafuatayo:

1- Kwa kutokwa na manii kwa matamanio.,

2- Kuota nywele sehemu za siri.

3- Kwa kuota usiku na akatokwa na manii.

4- Akafikisha miaka kumi na tano.

Mtoto wa kike anashirikiana na mtoto wa kiume katika mambo haya. Lakini yeye kuna kitu cha tano cha nyongeza alichonacho:

5- Hedhi.

Msingi wa hilo ni yale yaliyopokelewa na Imaam Ahmad na Abu Daawuud kutoka kwa ´Amr bin Shu´ayb, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake, aliyesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Waamrisheni watoto wenu swalah wanapokuwa na miaka saba, wapigeni kwayo wanapofikisha miaka kumi na watenganisheni katika vitanda.”

 ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anh) amepokea vilevile ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kalamu imesimamishwa kwa watu aina tatu; kwa aliye lala mpaka aamke, mtoto mpaka abaleghe na kwa mwendawazimu mpaka awe na akili.”

Ameipokea Imaam Ahmad na amepokea mfano wa hiyo kutoka katika upokezi wa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh). Ameipokea pia Abu Daawuud na at-Tirmidhiy ambaye amesema:

“Hadiyth ni nzuri.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/147-148)
  • Imechapishwa: 31/05/2017