Ni lini mtoto anatahiriwa?


Swali: Ni lini kunakuwa kutahiriwa?

Jibu: Mtu anaweza kutahiriwa pale anapotaka. Lakini bora ni kumtahiri kabla ya kubaleghe kama jinsi walivyokuwa wakifanya waarabu ili mtoto asije kubaleghe isipokuwa ameshatahiriwa. Kuhusu kumtahiri mtoto anapokuwa na miaka saba kuna maoni mawili ya wanachuoni. Ahmad ana maoni yote mawili ambapo katika moja wapo amesema kwamba haichukizwi kwa kuwa Ibraahiym alimtahiri Ishaaq alipokuwa na miaka saba na katika maoni mengine anaonelea kuwa inachukizwa kwa kuwa ni kitendo cha mayahudi na kwamba imechukizwa kujifananisha na wao. Haya ni maoni ya Maalik vilevile.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/113)
  • Imechapishwa: 19/11/2017