Swali 100: Ni lini mtawala anahukumiwa ukafiri wake? Ni lini itafaa kumfanyia uasi?

Jibu: Atahukumiwa ukafiri atapofanya jambo la kuritadisha kwa yeye kufanya moja katika vichenguzi vya Uislamu. Kama mfano wa kumshirikisha Allaah, kumuomba mwengine asiyekuwa Allaah na kumchinjia mwengine asiyekuwa Allaah. Akihukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah huku anaona kuwa ndio bora, kwamba ana khiyari ya kuhukumu na kanuni na Shari´ah, huyu anakuwa kafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema wakati alipoulizwa juu ya wale wataokuja katika zama za mwisho, wanafanya vibaya katika matendo yao na katika mienendo yao na wanawakandamiza watu, wakamuuliza Mtume wa Allaah kama itafaa kupambana nao ambapo akasema:

“Hapana, muda wa kuwa wanasimamisha swalah.”

Kwa sababu katika Khawaarij kuna makubwa zaidi kuliko yale ambayo wao wametumbukia ndani yake. Kusubiri juu ya maudhi yao ni jambo ambayo lina madhara pasi na shaka. Lakini yale yatayopelekea katika kuwafanyia uasi ni makubwa zaidi katika mpasuko, kufarikisha umoja wa waislamu na kuwasalitisha makafiri juu ya waislamu. Haya ni makubwa zaidi kuliko kustahamili dhuluma za mtawala mkandamizi au ambaye ni mtenda madhambi ambaye madhambi yake hayajafikia kiwango cha ukafiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 272
  • Imechapishwa: 14/11/2019