Ni lini msichana anaamrishwa kuvaa Hijaab?

Swali: Ni lini tunawaamrisha wasichana wetu kuvaa Hijaab?

Jibu: Ni lazima kuwaamrisha kuvaa Hijaab pindi wanapobaleghe. Pindi msichana anapofikisha miaka kumi na tano, akabaleghe kwa kutokwa na manii usingizini au nje ya usingizini au nywele zikaota sehemu ya siri.

Lakini inatakiwa kumpa mazoezi ya haya kabla ya hapo. Anapokaribia kufikisha miaka tisa basi hapo msichana huanza kuona haya. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Mkajazi anapofikisha tisa basi ni mwanamke.”

Kwa hiyo ni lazima hapo kuanza kumpa mazoezi ya Hijaab na kumuuasi kuvaa Hijaab. Lakini mtu afanye hivo bila ya kumfanyia ukali. Mpaka pale atapobaleghe atakuwa amekwishaizowea Hijaab. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah haikubali swalah ya mwenye hedhi isipokuwa akiwa na mtandio.”

Ni lazima kuvaa mtandio ndani ya swalah wakati anapobaleghe.

Yale yanayowahusu wanaume kitendo cha wao kuwasitirisha kabla ya wao kubaleghe, akazowea jambo hilo na akamwamrisha jambo hilo ndio jambo la aula na bora zaidi. Yote hayo ni kwa sababu ya kumweka mbali na khatari. Atapobaleghe itakuwa ni lazima kwake na atatakiwa kumlazimisha jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/17222/%D9%85%D8%AA%D9%89-%D8%AA%D9%88%D9%85%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%A8%D9%86%D8%A7%D8%AA-%D8%A8%D8%A7%D9%84%D8%AD%D8%AC%D8%A7%D8%A8
  • Imechapishwa: 22/01/2020