Ni lini mgonjwa anatakiwa kulisha na kutolisha Ramadhaan?

Swali: Mama yangu amepatwa na maradhi ya saratani ya damu mwanzoni mwa siku za mwezi wa Ramadhaan iliyopita na hakuweza kufunga mwezi mzima, hivyo akawa amelisha katika kila siku moja za mwezi huu. Je, kulisha huku kunamtoshelezea tu au ni lazima kwake kulipa siku hizi pamoja na kulisha pamoja na kujua ya kwamba hali yake imekuwa bora kwa hivi sasa?

Jibu: Ikiwa ni maradhi ambayo yanatarajiwa kupona, ni lazima kwake kulipa [kwa kufunga] na haitoshelezi kwake kulisha. Ama ikiwa ni maradhi ambayo hayatarajiwi kupona, katika hali hii inatoshelezi kulisha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (46) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-04-01.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014