Ni lini maamuma wanatakiwa kuitikia “Aamiyn”?

Swali: Wakati imamu atapomaliza kusema:

صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ

“Njia ya wale Uliowaneemesha si ya walioghadhibikiwa wala waliopotea.” (01:07)

Ni lini maamuma wanatakiwa kuitikia “Aamiyn”? Je, wasubiri mpaka aiseme kwanza imamu?

Jibu: Hapana. Imamu atapomaliza kusoma al-Faatihah ndipo aseme “Aamiyn”. Hakuna neno hata kama imamu atatangulia kusema “Aamiyn”.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (49) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/m-3%20%20-%2012%20-%202%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 04/11/2018