Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

34- Abu Sa’iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu´anh) ameeleza kuwa amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Yeyote yule atakayeona kitendo kiovu akiondoshe kwa mkono wake.”

Wanachuoni wametofautiana katika kauli mbili juu ya kwamba ni lazima kukataza maovu mtu akiwa na dhana yenye nguvu kuwa mnasihiwaji atapokea nasaha au hapana?

1- Kundi la kwanza la wanachuoni wanasema kuwa ni wajibu kukataza kwa kuwa ndio asli na hakuna dalili yoyote inayotoa masuala haya katika asli yake. Hii ni moja katika kauli mbili ilio na nguvu zaidi ya Imaam Ahmad (Rahimahu Allaha). Vilevile ndio kauli ya wanachuoni wengi.

2- Kundi la pili la wanachuoni wanasema kuwa mtu akiwa na dhana yenye nguvu kuwa mtu hatonufaika kwa kumkataza, itakuwa inapendekezwa kwake kumkataza na sio wajibu. Inaonekana kana kwamba Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ameshikamana na maoni haya. Ametolea dalili ya hilo Kauli Yake (´Azza wa Jall):

فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ الذِّكْرَىٰ

“Basi kumbusha ikiwa kunafaa ukumbusho.” (87:09)

Bi maana kumbusha ikiwa kama kukumbusha kutanufaisha. Hapo ndipo Amewajibisha kukumbusha.

Kunaingia katika hili vilevile mambo ya kukataza mtu akiwa na dhana yenye nguvu kuwa mkumbushwaji atanufaika nalo. Naonelea kuwa kauli hii ndio iko wazi na sahihi zaidi.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 466-467
  • Imechapishwa: 12/05/2020