Ni lini inalazimika kuleta Tasmiyah?

Swali: Ni wakati gani inalazimika kusema ”Bismillaah”?

Jibu: Wakati wa kuanza kula.

Swali: Mahali hapa peke yake?

Jibu: Mwazoni mwa kula, pia wakati wa kutawadha na wakati wa kuingia nyumbani. Sehemu zote hizi imewekwa katika Shari´ah na wakati wa kwenda kulala:

بِاسْمِكَ رَبِّـي وَضَعْـتُ جَنْـبي، وَبِكَ أَرْفَعُـه، فَإِن أَمْسَـكْتَ نَفْسـي فارْحَـمْها، وَإِنْ أَرْسَلْتَـها فاحْفَظْـها بِمـا تَحْفَـظُ بِه عِبـادَكَ الصّـالِحـين

”Kwa jina lako, Mola wangu, nimeweka ubavu wangu na kwa ajili Yako nitaunyanyua. Ukiizuia roho yangu, basi irehemu, na ukiirejesha, basi ihifadhi kwa yale unachowahifadhi kwayo waja Wako wema.”[1]

[1] al-Bukhaariy (11/126) na Muslim (04/2084).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21686/ما-المواضع-التي-تجب-فيها-التسمية
  • Imechapishwa: 16/09/2022