Ni lini inakuwa wajibu kuhudhuria karamu ya ndoa na lini sio wajibu?


Swali: Ni ipi hukumu ya kuitikia karamu ya ndoa wa harusi ya muislamu? Je, yule asiyehudhuria anakuwa amemuasi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Vipi ikiwa kutakuwa maovu itakuwa bado ni wajibu kwangu kuhudhuria au hapana?

Jibu: Msingi ni kuitikia wito.

“… na anapokualika, basi muitikie.”

Miongoni mwa haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake:

“… na anapokualika, basi muitikie.”

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Shari ya chakula ni chakula cha walima. Wanaalikwa matajiri na wanatengwa mafukara. Na yule asiyeitikia basi amemuasi Allaah na Mtume Wake.”

Lakini ikiwa kutakuwa maovu na wewe huwezi kuyaondosha, haijuzu kwako kuhudhuria. Ikiwa kuna maovu na wewe huwezi kuyaondosha, basi haijuzu kwako kuhudhuria.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13694
  • Imechapishwa: 20/09/2020