Ni lini inaisha Takbiyr ya ´Iyd-ul-Fitwr?

Swali: Ni lini inaisha Takbiyr ya ´Iyd?

Jibu: Inaisha pale ambapo imamu anapohudhuria katika swalah. Pale wanapoanza kuswali imamu anafanya Takbiyr, na yeye pia atafanya Takbiyr mwanzoni mwa swalah na mwanzoni mwa Khutbah. Ama kuhusu waswaliji, Takbiyr yao inaisha wakati imamu anapokuja katika kiwanja cha swalah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/%205843
  • Imechapishwa: 03/05/2015