Ni lini inaanza Takbiyr ya ´Iyd na namna yake?


Swali: Ni lini inaanza Takbiyr ya ´Iyd? Ni ipi namna yake?

Jibu: Takbiyr ya ´Iyd inaanza ile siku ya mwisho ya Ramadhaan pale tu kunapozama jua mpaka pale imamu anapofika katika swalah ya ´Iyd. Namna yake ni kusema:

الله أكبر الله أكبر، لا إله إلا الله، والله أكبر، الله أكبر ولله الحمد،

“Allaah ni mkubwa! Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah! Allaah ni mkubwa!  Allaah ni mkubwa na himdi zote anastahiki Allaah!”

Au aseme:

الله أكبر، الله أكبر، الله أكبر، لا إله إلا الله، والله أكبر، الله أكبر، الله أكبر، ولله الحمد،

 “Allaah ni mkubwa! Allaah ni mkubwa! Allaah ni mkubwa! Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah! Allaah ni mkubwa!  Allaah ni mkubwa! Allaah ni mkubwa na himdi zote anastahiki Allaah!”

Kwa msemo mwingine mtu anaweza kusema Takbiyr mara tatu au mara mbili. Zote zinafaa.

Inatakiwa kudhihirisha nembo hii na watu waiseme kwa sauti ya juu masokoni, misikitini na majumbani. Kuhusu wanawake bora kwao waiseme kimyakimya.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawa (16/259)
  • Imechapishwa: 14/06/2018