Ni lini anazingatiwa amewahi Rak´ah katika swalah ya kupatwa kwa jua?


Swali: Niliiwahi swalah ya kupatwa kwa jua katika Rukuu´ ya pili katika Rak´ah ya kwanza. Je, nahesabika nimewahi Rak´ah?

Jibu: Swalah ya kupatwa kwa jua ina Rak´ah mbili ambapo kila Rak´ah moja ina Rukuu´ mbili. Akiwahi ile Rukuu´ ya kwanza amewahi Rak´ah. Akipitwa na ile Rukuu´ ya kwanza amepitwa na Rak´ah. Kujengea juu ya haya akijiunga pamoja na imamu baada ya yeye kuinuka katika ile Rukuu´ ya kwanza basi amepitwa na Rak´ah. Hivyo anatakiwa kuilipa pale imamu atapopiga Tasliym.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (77) http://binothaimeen.net/content/1765
  • Imechapishwa: 13/09/2020