Ni lini anaanza na kumaliza mwenye kukaa I´tikaaf?

Kuhusu masuala ya I´tikaaf mtu anaanza I´tikaaf pindi jua linapozama ile tarehe ishirini. Kwa msemo mwingine pale unapoanza usiku wa tarehe ishirini na moja. Anamaliza I´tikaaf kwa kuzama kwa jua ile siku ya mwisho ya Ramadhaan. Ni mamoja ni tarehe ishirini na tisa au thelathini. Anaenda nyumbani kwake. Hakuna haja ya yeye kubaki msikitini mpaka kwanza atoke aende kuswali swalah ya ´Iyd. Haya – japokuwa yamesemwa na baadhi ya wanachuoni – hayana dalili.

Jengine ni kwamba yule mwenye kufanya I´tikaaf atoke kama wengine akiwa na mavazi mazuri. Mambo si kama walivosema baadhi yao kwamba atoke akiwa na zile nguo anazofanyiwa I´tikaaf kwa madai kwamba zina athari ya ´ibaadah kama damu ya shahidi inavyobaki kwake. Sisi tunasema kuwa nguo hazina athari ya I´tikaaf. I´tikaaf haibadilishi chochote katika mavazi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (71) http://binothaimeen.net/content/1644
  • Imechapishwa: 01/04/2020