Ni lazima ovu likatazwe papohapo?


Swali: Je, inafaa kuchelewesha kumkataza mtu ambaye ametumbukia kwa mfano ndani ya shirki, ukafiri au haramu nyingine ili kufikia manufaa fulani au kuepuka madhara yaliyo makubwa zaidi?

Jibu: Allaah (Ta´ala) amesema:

ادْعُ إِلِى سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ

“Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima.”[1]

Ni lazima kuwa mwenye hekima. Ikiwa mtu anaona kuwa bora ni kusubiri kidogo na asianze kumkataza, kufanya hivo ni vizuri.

[1] 16:125

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (7 A)
  • Imechapishwa: 10/06/2021