Ni lazima mwanamke awe na Mahram katika Hajj na ´Umrah

Swali: Mwanamke akitaka kwenda katika ´umrah au katika hajj ya wajibu ni lazima aandamane na Mahram au anaweza kwenda peke yake?

Jibu: Ni lazima aandamane na Mahram katika hajj na safari nyenginezo:

“Si halali kwa mwanamke anayemuamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Kuhusu hajj asipopata Mahram asubiri mpaka pale atapopata. Vinginevyo endapo atakata tamaa ya kupata Mahram basi amuwakilishe mtu atakayemfanyia hajj.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (83) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-15-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 12/01/2018