Ni lazima mtu airudi swalah aliyoswali kabla ya muda kuingia?

Swali: Nikiswali faradhi moja wapo takriban dakika 10 na hayo yametokana na kusahau kwangu. Je, swalah hiyo imekwishapita kwangu au bado iko katika dhimma yangu?

Jibu: Ukiiswali kabla ya wakati inakuwa batili na wala haidondoki kutoka katika dhimma yako. Ukiswali Dhuhr kabla ya jua kupinduka, Maghrib kabla ya jua kuzama au Fajr kabla ya kuingia alfajiri ya kweli basi swalah inakuwa batili. Ni lazima kwako kuirudi na wala haitoki katika dhimma yako isipokuwa kwa kuirudi.

Haijuzu kwako kabisa kuswali kabla ya wakati. Unapata dhambi. Ni lazima utubu juu ya tendo hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/11014/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%AA%D8%A7%D8%AF%D9%8A%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D9%82%D8%A8%D9%84-%D8%AF%D8%AE%D9%88%D9%84-%D8%A7%D9%84%D9%88%D9%82%D8%AA
  • Imechapishwa: 25/04/2020